.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 13 Agosti 2016

SWANSEA NA WEST BROM WAANZA KWA USHINDI FINYU LIGI KUU YA UINGEREZA

Goli la dakika za mwisho la Leroy Fer limeipatia Swansea ushindi dhidi ya Burnley katika moja ya michezo ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa msimu huu.

Golikipa wa Burnley, Tom Heaton alishindwa kuudaka mpira wa krosi uliopigwa na Jefferson Montero ambao ulimkuta Fer aliyeutumbukiza golini.
    Leroy Fer akipachika wavuni goli pekee katika mchezo huo na kuipatia Swansea ushindi
Katika mchezo mwingine goli la mpira wa kichwa lililofungwa na Solomon Rondon lilitosha kuipatia West Brom ushindi mwembamba dhidi ya Crystal Palace katika dimba la Selhurst Park.

Andros Townsend alishindwa kuonyesha makali yake katika mchezo huo wakati akiichezea kwa mara ya kwanza timu ya Crystal Palace akitokea Newcastle.
Solomon Rondon akiwa juu hewani na kupiga mpira wa kichwa uliojaa wavuni na kuipa ushindi West Brom

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni