Waziri
kijana kuliko mawaziri wote waliowahi kuteuliwa nchini Sweden, Aida
Hadzialic, amejiuzulu baada ya kukutwa akiendesha gari huku akiwa na
kiwango kikubwa cha pombe mwilini.
Waziri
Hadzialic, 29, ni Waziri wa Elimu ya Juu katika serikali ya mrego wa
kati wa kushoto na ni waziri wa kwanza Muislam nchini Sweden.
Hadzialic
amesema kitendo chake hicho cha kuendesha gari huku akiwa amelewa ni
kosa kubwa katika maisha yake.
Hadzialic,
ambaye alihamia nchini Sweden akiwa na umri wa miaka 5 akitokea
Bosnia-Hercegovina, alikunywa glasi mbili za wine kabla ya
kusimamishwa katika daraja linalounganisha Denmark na Sweden.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni