.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 27 Septemba 2016

TAMWA YATAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUTOA FURSA YA WANAWAKE KUSIKIKA


Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu, wakiwa kwenye semina iliyofanyika Jumamosi wiki iliyopita Septemba 23, 2016 Jijini Dar es salaam. Semina hiyo iliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, ambapo pamoja na mambo mengine iliangazia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari kuhusu mafanikio na changamo za wanawake ili kufanya jamii iwatambue na hivyo kuwafunguliwa fursa mpya ikiwemo kujitokeza kwenye masuala ya uongozi. (Picha na BMG)


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, Alakok Mayombo, akifungua semina hiyo.
Kushoto ni mkufunzi katika semina hiyo, Valerie Msoka ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya InterNews tawi la Tanzania. Pia ni Mkurugenzi mstaafu wa TAMWA.

Godfrida Jola ambaye ni Afisa Miradi TAMWA, akizungumza jambo kwenye semina hiyo
                                                                     Mshiriki akichangia jambo 
                                                                          Washiriki wa semina hiyo




                                      Mmoja wa wanasemina akichangia jambo

                                                        Wanasemina kwenye majadiliano

                                                       Wanasemina kwenye majadiliano    Wanasemina kwenye majadiliano


                                 Makabidhiano ya nakala mbalimbali kutoka TAMWA



Kulia ni Godfrida Jola kutoka TAMWA na kushoto ni George Binagi-GB Pazzo kutoka Lake Fm Mwanza & BMG.

Na. BMG
Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kutoa fursa kwa wanawake kuonesha umahiri wa utendaji wao wa kazi ili kuleta chachu kwa wanawake wengi zaidi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, Alakok Mayombo, alitoa rai hiyo jumamosi iliyopita kwenye mafunzo kwa wanaandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu yaliyofanyika jijini dar es salaam.

Alisema bado idadi ya wanawake walio kwenye nafasi mbalimbali za uongozi serikalini ni chini ya asilimia 30 kwa nchi za kusini mwa Bara la Afrika ikiwemo Tanzania hivyo waandishi wa habari wana nafasi kubwa kuwahamasisha wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yaliandaliwa na TAMWA, walisema mafunzo hayo yawatawasaidia kuandaa vipindi bora vitakavyowahamasisha wanawake nchini kujitokea kuwania nafasi za uongozi katika jamii.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni