Na MahmoudAhmad Arusha
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingiza imewataka wakazi wa jiji la Arusha kukaa mkao wa kula kwani wapo katika wakati wa kuboresha huduma zake kwenye kipindi cha miaka miwili na nusu iliyobakia katika uboresha wa miundombinu na utafutaji wavyanzo vipya vya maji na kuwa tatizo la maji litakuwa historia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa AUWSA Ruth Koya wakati akijibu maswali ya wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Mkutano wa maboresho ya mkataba wa huduma kwawateja jijini Arusha.Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya upungufu wa maji kwa mda mrefu na serikali imeliona
hilo ndio maana ikatenga kiasi cha tsh,476 bilion za uboreshaji wa huduma mbali mbali za mamlaka hiyo hivyo suala hilo linafanyiwa kazi kuanzia mwaka huu hadimwaka 2018 litakapokamilika.
“Tuwe na subra maradi huu kwa sasa una mda wa miezi nane tangia uanze na mkandarasi wa utafutaji wa vyanzo vya maji yupo kazi akishakamilisha tutaanza maboresho yamiundombinu yetu ilkuweza kuwafikishia maji kwa wateja wetu wote”alisema Koya.
Kwa upande wake kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Afisa tarafa wa jiji la Arusha Felician Rutehengerwa aliitaka Auwsa kuwabainisha wezi wote wa maji ilikuweza kuwafisha katika mikono ya kisheria kwani suala hilo pia linachangia wananchikukosa huduma ya maji safi na upotevu wa maji.
Alisema kuwa kumekuwapo na vyanzo vingi vya maji zaidi ya 19 na vingine vimeanzishwa na viwanda ambavyo vimekuwa vikiikosesha Auwsa mapato ikiwemo kiwanda cha A to Z ambacho kimekuwa kikigawa maji bure
huku wakitambua kuwa wao hawana mamlaka ya kisheria ya usimamizi wa maji hivyoni mteja mkubwa mnampoteza kulipa huduma za maji.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Job Laizer alisema kuwa Malalamiko ambayo wananchi wameyatoa ni changamoto kubwa kwao katika kuifanya mamlaka hiyo kuboresha huduma zake na kuwaahidi wadau kuyasimamia na kuahkikisha wateja wanapatahuduma bora na kwa wakati.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni