Barcelona imeshindwa kupunguza pengo
na vinara wa La Liga Real Madrid baada ya kulazimishwa sare ya goli
1-1 na Atletico Madrid.
Baada ya kushindwa kuipenya ngome ya
Atletico kwa pasi, wenyeji Barcelona walipata goli la kuongoza
kupitia kwa Ivan Rakitic akiunganisha kwa kichwa krosi ya Andres
Iniesta.
Katika mchezo huo Lionel Messi
alilazimika kutoka nje baada ya kuumia na Atletico walitumia fursa
hiyo kwa kusawazisha kupitia kwa Angel Correa.
Ivan Rakitic akiwa amepiga mpira wa kichwa uliotinga wavuni
Lionel Messi akigugumia maumivu baada ya kuumia ambapo imeelezwa atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki tatu hivi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni