Mwanzo mzuri wa Mario Balotelli
akiwa na klabu ya Nice umeendelea baada ya mchezaji huyo kutundika
magoli mawili wakati wakiizamisha Monaco kwa magoli 4-0 katika mchezo
wa Ligi 1.
Mshambuliaji huyo raia wa Italia
alifunga magoli mawili katika mchezo wake wa kwanza tangu ahamie Ligi
ya Ufaransa, na jana tena alifumania nyavu katika vipindi vyote viwili.
Magoli mengine ya Nice yalifungwa na
Paul Baysse aliyefunga la kwanza, huku Alassane Plea akikamilisha la
nne na kuifanya Nice kuchuma pointi 14 katika michezo sita.
Mario Balotelli akiachia shuti na kuandika goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni