Real Madrid imepoteza nafasi ya
kuvunja rekodi ya kushinda michezo 17 mfululizo katika Ligi ya La
Liga baada ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Villarreal.
Wenyeji Madrid walijikuta wakifungwa
goli baada ya Sergio Ramos kuuzuia kwa mkono mpira na Bruno Soriano
kufunga kwa mkwaju wa penati.
Hata hivyo baadaye Sergio Ramos
alirekebisha makosa yake baada ya tu ya kuanza kipindi cha pili kwa
kufunga kwa kichwa mpira wa kona.
Sergio Ramos akiwa ameupiga mpira kwa kichwa ambao ulienda kujaa wavuni
Cristiano Ronaldo alidhibitiwa vilivyo na kushindwa kutikisa nyavu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni