.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Septemba 2016

CHELSEA LICHA YA KUSHINDWA KUPATA USHINDI JANA YAMPOTEZA KAPTENI WAKE

Chelsea sio tu imeshindwa kupata pointi tatu baada ya kupambana kiume na Swansea na kutoka sare ya magoli 2-2, bali pia mchezo huo umeamuacha na hofu kocha wao Antonio Conte.

Hii ni baada ya kapteni wa klabu hiyo John Terry, kujikuta akipata jeraha la kwenye enka katika dakika za mwisho za mchezo huo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

John Terry alikwatuliwa na mshambuliaji matata Leroy Fer, aliyeifungia Swansea goli na kumfanya beki huyo aruke juu na kuumia. 
                    Kapteni wa Chelsea John Terry akigugumia maumivu baada ya kukwatuliwa 
     Kapteni John Terry akiwa na fimbo maalum za kumsaidia kutembe baada ya kuumia

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni