.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Septemba 2016

DC BUSEGA AWACHARUKIA WAVUVI HARAMU

Mkuu wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Bi Tano Mwela akisitiza jambo kwa wavuvi.
Afisa uvuvi wilaya ya Busega akionyesha kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani ) nyavu haramu ambazo hazikubaliki kwa uvuvi.

                                                                                            Na Shushu Joel,BUSEGA.

MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu Bi Tano Mwela amewacharukia wavuvi wanaotumia zana haramu katika wilaya hiyo kuzisalimisha mara moja ndani siku kuni.

Akizungumza na wavuvi katika Kijiji cha Nyamikoma mwalo wa Fogofogo, Mwela alisema wavuvi hao wawe wamesalimisha zana hizo hadi ifikapo tarehe 17 mwezi huu katika ofisi za BMU, na kwamba atakayekaidi atakumbana na mkono wa sheria.

Mwela alitumia fursa hiyo kuwaonya waliozoea kufanya kazi kwa mazoea kuacha mara moja kwani katika utekelezaji wa jambo hili hakutakuwa na mazaha.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ameyatupilia mbali maombi ya wavuvi hao ya kutaka waongezwe muda wa mwezi mmoja wajipange kwa kusema suala la uvuvi haramu ni la miaka mingi lakini watu wameziba pamba masikioni.

“Jambo jingine ambalo napenda kusisitiza ni juu ya mabwana masamaki ambao wanakuwa wakishilikiana na wavuvi haramu katika kazi zao kwa kutoa taarifa, tutakayembaini atakwenda na maji”

Kwa upande wao wavuvi wa wa eneo hilo wakiongozwa na Samwel Juma walimuomba mkuu huyo wa wilaya awaongeze siku za kuendelea na uvuvi ili waweze kupata mtaji wa kununua nyavu zinazokubalika za mm 8, lakini mkuu huyo wa wilaya alitupilia mbali ombi hilo.

Hata hivyo wavuvi wa sangara walimpongeza hatua hiyo ya mkuu wa wilaya kwa kusema inalenga kulinda mazalia ya samaki katika ziwa Victoria.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni