.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Septemba 2016

DTB KUSAINI MKATABA NA TFF

Benki inayokuja juu katika soko la fedha nchini Tanzania ya DTB (Diamond Trust Bank), kesho Jumatatu saa 4.30 asubuhi inatarajiwa kusaini mkataba wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuongeza udhamini katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hafla ya kusaini mkataba huo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, iliyoko kwenye makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Ohio jijini Dar es Salaam. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wanakaribishwa kwenye hafla hiyo itakayofanyika hotelini hapo.


WAPENZI WA SOKA KUNUFAIKA NA ‘SOKA BANDO’

Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara , “Vodacom Premier League” imesikia kilio cha mashabiki na wapenzi wa soka nchini na kuamua kuwaletea kifurushi maalumu kinachojulikana kama ‘Soka bando’ ambacho ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote.

Vodacom Tanzania imebuni kifurushi hiki kwa ajili ya kuwapatia taarifa za soka za hapa nchini na ligi za kimataifa kwa gharama nafuu ya shilingi 500/-Kifurushi cha ‘Soka bando’ kitakuwa kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa masaa 24.
 

                                                    Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
 

http://tff.or.tz/news/598-wapenzi-wa-soka-kunufaika-na-soka-bando

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni