Gerard Pique ameisaidia Barcelona
kuongoza kundi C baada ya kuifungia goli la ushindi katika kipindi
cha pili na kufanya matokeo kuwa 2-1 dhidi ya Borussia
Monchengladbach.
Timu hiyo ya Ujerumani ilipata goli
la kuongoza dhidi ya Barcelona, katika kipindi cha kwanza kupitia kwa
Thorgon Hazard.
Barcelona ilirejesha uhai wake baada
ya kusawazisha kupitia kwa Arda Turan na kisha baadaye Pique kufunga
la pili.
Beki Gerard Pique akifunga goli la pili lililoipa ushindi Barcelona
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni