Sam Allardyce ameachia madaraka ya
ukocha wa Uingereza baada ya kuafikia makubaliano na Chama cha Soka
Uingereza (FA) baada ya kuiongoza timu hiyo katika mchezo mmoja na
kuwa nayo kwa siku 67 tu.
Hatua hiyo inafuatia habari ya
uchunguzi ya gazeti la Telegram ambao inadai kuwa Allardyce, 61,
alitoa ushauri wa jinsi ya kukwepa sheria za FA kuhusiana na uhamisho
wa mchezaji.
Allardyce, anadaiwa kutumia nafasi
yake kuzungumzia mpango wa kujipatia kiasi cha paundi 400,000
kuiwakilisha kampuni moja ya Mashariki ya Mbali.
Katika taarifa yake Cama cha Soka
FA, kimesema alichofanya Allardyce si jambo sahihi, na kwa sasa
Gareth Southgate ataiongoza kwa muda timu ya taifa ya Uingereza.
Ni kama anasema "Mungu wangu nimefanya nini tena hiki jamani".
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni