.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 28 Septemba 2016

LHRC WASHEREHEKEA MIAKA 21 NA WATOTO WANAOISHI MAKAO YA TAIFA YA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

Wafanyakazi wa LHRC wakijumuika na watoto wanaolelewa katika Makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 21 tangu kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati) akiwasaidia watoto kukata keki kusheherekea miaka 21 ya LHRC.
Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.


                                                                                                              Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba serikali kupitia wizara ya Afya ,Jamii Jinsia ,Wazee na Watoto, pamoja na na Wizara ya Katiiba na Sheria ,kufanya marekebisho yaSsheria ya Mtoto nakutilia mkazo malezi bora ya watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakacho toa adhabu kali kwa familia itakayo shindwa kutoa malezibora kwa watoto au kutelekeza familia.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 21 ya kituo cha sheria na haki za binadamu, yaliyofanyika katika Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida kilichopo Kurasini, Temeke Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dk. Helen Kijo-Bisimba alisema kuboreshwa kwa sheria hizo kutasaidia kupunguza wimbi la watoto wasio na makao maalumu wanao zagaa kuomba omba mitaani, na ameitaka jamii kushiriki katika kutatua tatizo la watoto wa mitaani linalozidi kushika hatamu kila siku.

Ofisa Mfawidhi wa kituo hicho, Beatrice Laurence ame kishukuru kituo cha sheria na haki za Nina damu kwakuona umuhimu wa kutoka misaada katika kuwa saidia watoto wanao lelewa hapo nakuwataka watanzania wengine badala ya kuelekeza nguvu zao pekee kwa wathirika wa tetemeko huko Kagera kuwa kumbuka na watoto yatima kwani nao wanayo kahitaji ya kibinadamu.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzishwa Septemba 26, 1995 kwa lengo la kufanya utetezi kwa watu wenye uhitaji sambamba na kulinda haki za binadamu nchini. 


( Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062 )

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni