.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 2 Septemba 2016

LIGI KUU YA VODACOM, MECHI NNE KESHO



Raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 3, 2016 kwa michezo minne wakati kwa Jumapili Septemba 4, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TBLB).

Michezo ya kesho ni kati ya Mbao FC na Mbeya City utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Kagera Sugar itazindua uwanja wa nyumbani kwa kucheza na Mwadui ya Shinyanga.

Majimaji itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea na African Lyon itakuwa mgeni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

Mchezo wa Jumapili utakuwa ni kati ya Stand United na Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Ligi hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Azam FC itaendelea Jumatano kwa michezo mitatu ambako mabingwa watetezi Young Africans watakaribishwa na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Azam ambayo kwa sasa inangoza ligi hiyo itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine ilihali Simba itakipiga na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

TAIFA STARS KAZINI KESHO

Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kesho Septemba 3, 2016 inatarajiwa kuingia kibaruani kwa kucheza na Super Eagles ya Nigeria katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Mchezo huo utafanyika kuanzia saa 11.00 (17h00) jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabo, mjini Uyo katika Jimbo la Akwa Ibom. Muda huo uko mbele kwa saa mbili kamili kwa maana hiyo Taifa Stars itacheza dhidi ya Nigeria saa 9.00 alasiri (15h00).

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini


http://tff.or.tz/news/571-taifa-stars-kazini-kesho-jumamosi

MWISHO WA KUJISAJILI GPX NI JUMATATU

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kwa mara nyingine, limeagiza klabu tisa za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Klabu sita za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (TFDL) kujiunga mara moja na mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji.

FIFA imeiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), likitaja klabu tisa za VPL na TFDL kujisajili kabla ya Jumatatu wiki ijayo kwani itasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji ambayo timu itahitaji kumsajili. Lengo ni kurahisisha mawasiliano ya usajili kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System).

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

http://tff.or.tz/news/570-klabu-zatakiwa-kujisajili-gpx-kabla-ya-jumatatu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni