.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Septemba 2016

MAMA TERESA KUTANGAZWA MTAKATIFU LEO VATICAN

Mtawa Mama Teresa, ambaye anajulikana zaidi kwa kujitolea katika kuwasaidia masikini nchini India, atatangazwa kuwa mtakatifu hii leo Jijini Vatican.

Makumi kwa melfu ya watu wamekusanyika katika eneo lawazi la Kanisa la Mtakatifu Peter kushuhudia Papa Francis akiongoza hafla hiyo ya kutangazwa Mtakatifu Mama Teresa.

Kuridhiwa utakatifu wa Mama Teresa kunafuatia ushuhuda wa miujiza miwili ya kutibu wagonjwa aliyofanya Mama Teresa, baada ya kifo chake.

Watu 1,500 wasio na makazi nchini Italia wamepelekwa kwa mabasi Jijini Roma kushuhudia hafla hiyo, na watapatia mlo wa mchana wa pizza na watawa 250 wa Taasisi ya Masista.
                                      Watawa wa Taasisi ya Mama Teresa wakiwasili Vatican

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni