.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 20 Septemba 2016

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SEREKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO

MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa
shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliouthuria mkutano huo

                                                                       Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la
Arusha Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .

Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa
shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na
kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya
likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila siku madeni hayo.

“mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe.

Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .

Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati
wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu bora.

Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na
tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku
wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja
bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.





Wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao


Picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni