.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Septemba 2016

NEYMAR AIFUNGIA BRAZIL GOLI LA USHINDI DHIDI YA COLOMBIA

Goli la kipindi cha pili la Neymar limeipatia Brazil ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Colombia na kuifanya kupata ushindi wa pili katika michezo ya kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia 2018.

Wenyeji Brazil walianza vyema kwa kupata goli baada ya sekunde 80 tu Miranda aliporuka juu na kufunga kwa mpira wa kichwa ikiwa ni goli lake la kwanza kuifungia Brazil katika michezo 33 aliyoichezea.

Brazil ikiwa chini ya kocha Tite, ilikitawala kipindi cha kwanza kwa pasi safi, lakini hata hivyo Colombia ilifanikiwa kusawazisha goli katika dakika ya 35, lakini Neymar aliipatia Brazil goli la pili katika kipindi cha pili.
                           Mchezaji tegemeo wa timu ya Brazil Neymar akifanya vitu vyake 
                                                   Kocha Tite akimkumbatia Neymar kumpongeza

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni