.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Septemba 2016

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN ATUMA SALAAM ZA RAMBIRAMBI KWA WANANCHI WA MKOA WA KAGERA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo na maafa mengine vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana Septemba 10, 2016 majira ya laasiri katika Mkoa wa Kagera pamoja na maeneo mengine ya jirani.

Kufuatia tukio hilo Rais wa Zanzibar anaungana na familia zote zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki na anawaombea marehemu wapumzishwe mahala pema panapostahiki na awape subira ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu hao katika kipindi hiki kigumu.

Aidha, Dk. Shein amewaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi wote walioathirika kutokana na tetemeko hilo wapone haraka na kurejea katika hali zao za kawaida ili waweze kufanya shughuli zao za kila siku kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.

Wananchi wa Zanzibar wanaungana Mkuu wa Mkoa wa Kagera, wananchi wake pamoja na Watanzania wote kwa jumla katika kuomboleza msiba huo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni