.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 13 Septemba 2016

ROMELU LUKAKU APIGA HAT-TRICK WAKATI EVERTON IKIICHAKAZA SUNDERLAND

Romelu Lukaku amefunga magoli matatu yaani hat-trick ndani ya dakika 11, wakati Everton ikiendeleza rekodi yake ya kutofungwa tangu msimu huu uanze na kuibuka na ushindi dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji alifunga goli la kwanza kwa klabu yake tangu mwezi Machi, kwa mpira wa kichwa kufuatia krosi ya Idrissa Gueye na kisha kuongeza la pili kupitia pande la
Yannick Bolasie.

Lukaku alitundika goli la tatu kwa shuti la chini baada ya kutoka kasi na kuuwahi mpira, na kuihakikishia Everton ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Sunderland mbayo haijashinda mchezo wowote wakiwa chini ya kocha David Moyes.
                  Romelu Lukaku akiruka juu na kutumbukiza mpira wavuni kwa kichwa
           Kipa wa Sunderland akiwa ametumbukia wavuni baada ya kuteswa na Lukaku

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni