.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Septemba 2016

SERENA WILLIAMS APOTEZA NAFASI YA KUENDELEA KUWA NAMBA MOJA

Serena Williams amepoteza nafasi ya kwanza duniani aliyokuwa akiishikilia katika mchezo wa tenesi wanawake, baada ya kushindwa katika hali ya kushangaza mchezo wa nusu fainali za US Open dhidi ya raia wa Czech Karolina Pliskova.

Serena aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo ya tangu Februari 18, 2013, ameweza kuishikilia nafasi hiyo ya juu katika mchezo huo kwa wiki 186 mfululizo, ambayo ni sawa na rekodi iliyowekwa na Mjerumani, Steffi Graf.

Williams aliyepaswa kutinga fainali ili aweze kujipa nafasi ya kuweza kuvunja rekodi ya Graf, alijikuta akibugi mahesabu na kufungwa na mchezaji namba 10 Pliskova kwa seti 6-2, 7-6 (3) mbele ya umati wa watu Jijini New York katika mchezo uliochezwa kwa saa mbili na dakika 26.
                                               Karolina Pliskova akishangilia baada ya kushinda
                           Serena Williams akiinamisha kichwa chini baada ya kushindwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni