Timu ya kampeni ya mgombea urais wa
Marekani Donald Trump imeafiki kwa kwa mara ya kwanza kabisa kuwa
rais Barack Obama ni mzaliwa Marekani.
Mgombea huyo urais wa Republican
amekuwa kiongozi wa harakati za uzawa ambazo zilikuwa zikihoji rais
Obama ambaye alizaliwa Hawaii kama ni mzaliwa wa Marekani.
Kampeni ya Trump sasa imemtuhumu
mgombea urais wa Democratic Hillary Clinton kwa kuanzisha tuhuma hizo
kwa rais Obama katika mchakato wa kumpata mgombea wa urais mwaka
2008.
Hata hivyo hakuna ushahidi wowote
unaomhusisha moja kwa moja Hillary Clinton kushiriki harakati hizo za
uzawa ambazo ni za kibaguzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni