Mamlaka nchini Marekani imetoa wito
wa kuondolewa sokoni kwa simu aina ya Samsung Galaxy Note 7 baada ya
kuripotiwa kusababisha moto kutokana na kuwa hitilafu kwenye mfumo wa
betri.
Kampuni kubwa ya Korea Kusini
inayotengeneza simu hizo tayari nayo imetoa wito kwa watumiaji
waliokwishanunua simu hizo kuzirejesha baada ya kuibuka kwa
malalamiko kuwa zinalipuka moto.
Kwa mujibu wa kampuni ya Samsung,
tatizo hilo limeathiri simu za Samsung Galaxy Note 7 milioni 2.5 duniani ambapo nchini
Marekani pekee zipo simu milioni 1.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni