Klabu za Ligi Kuu ya Uingereza
zimetumia zaidi ya paundi milioni 155 katika siku ya mwisho ya
uhamisho na kuweka rekodi ya uhamisho wachezaji uliofikia kiasi cha
paundi bilioni 1.165.
Kabla ya kufikia jana timu za
Uingereza zilishakuwa zimetumia kiasi cha paundi bilioni 1.005, na
sasa uhamisho wa msimu huu wa majira ya joto, umevunja rekodi ya
mwaka jana ya paundi milioni 870.
Klabu 20 zinazoshiriki ligi kuu ya
Uingereza zimenufaika na makubaliano ya malipo ya televisheni
yaliyoweka rekodi ya paundi bilioni 5.1 kuanzia msimu huu.
Mchezaji wa Manchester United Paul Pogba uhamisho wake unaofikia paundi milioni 100 umeweka rekodi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni