WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali itapitia upya sababu za kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bonde la
Mto Rufiji (RUBADA) kufuatia mamlaka hiyo kuendeshwa kwa ubabaishaji.
Hatua hiyo imekuja baada ya mamlaka
hiyo kushindwa kusimamia uendelezaji wa bonde hilo na kusababisha
malalamiko kutoka kwa wananchi.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana
(Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika Ikwiriri mkoani Pwani.
Alisema baada ya mapitio hayo
shughuli za mamlaka hiyo zitahamishiwa kwenye mamlaka nyingine za
serikali kwani RUBADA imeshindwa kufanyakazi hiyo kwa muda mrefu.
“RUBADA wamepewa ardhi lakini
wameshindwa kuiendeleza, tutafanya upya mapitio ya kuanzishwa kwake,”
alisema.
Akizungumzia kuhusu Kampuni ya Agro
Forestry Plantation inayotaka kujenga kiwanda cha sukari wiyani
Rufiji aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha asilimia 60 ya watumishi
watakaowaajiri wawe ni vijana wa wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium
Lukuvi, kwenda wilayani Rufiji kutatua mgogoro wa mpaka kati ya
Wilaya ya Mkuranga na Ikwiriri.
Waziri Mkuu amelitoa agizo hilo
baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Ikwiriri kuhusu
kutotatuliwa kwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.
Naye Mkurugenzi wa halshauri ya
wilaya hiyo, Rashidi Salum alimweleza Waziri Mkuu kuwa, mgogoro huo
umeshatatuliwa kwa ngazi ya wilaya hivyo hatua iliyosalia ni kwa
uWaziri wa Ardhi kufika na ramani ili kutoa uamuzi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, SEPTEMBA 27, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni