Mkuu wa wilya ya Iringa, Richard Kasesela akishiriki kuuzima moto mkubwa uli0zuka katika uwanja wa ndege wa Nduli manispaa ya Iringa.
Mkuu wa wilya ya Iringa, Richard Kasesela akiliongoza gari la kikosi cha zima moto kwenda kuzima moto mkubwa uli0zuka katika uwanja wa ndege wa Nduli manispaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akishiriki kuzima moto mkubwa uliozuka katika uwanja wa ndege wa Nduli manispaa ya Iringa.
Moto mkubwa ulizuka katika uwanja wa ndege wa Nduli manispaa ya Iringa ambao ulisababishwa na uchomaji mashamba yaliyopo jirani na uwanja
huo.
Kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuzima moto huo ambao ungeweza
kuteketeza vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na majengo. Akizungumza katika
eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye alishirikiana na kikosi
cha zimamoto kuzima moto huo alisema " lazima wananchi wajue kutenga
mashamba yao kuzuia mioto kusambaa kuanzia sasa yoyote atakaye sababisha
moto kutoka kwenye shamba lake atachukuliwa hatua kali za kisheria.
"
Mkuu wa wilaya aliagiza manispaa itengeneze kwa kutumia bullodozer barabara
ya kuzuia moto kuzunguka uwanja. Moto huo ulianza majira ya saa 7 mchana
na kusambaa hadi kwenye uwanja wa kuondokea ndege (Runway) pia
kusogelea eneo la kuhifadhia mafuta ya ndege na vifaa vya kuongozea
ndege.
Ulidhibitiwa vizuri hadi kufikia saa 9.43 moto ulikuwa umezimwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni