Beki Vincent Kompany atafanyiwa
matibabu hii leo kwenye hospitali ya Jijini Barcelona akiwa na
mchezaji mwenzake wa Manchester City, Kevin De Bruyne, katika
kujaribu kupigania kupona tangu aumie misuli.
De Bruyne naye anatarajiwa kupatiwa
tiba maalum nchini Hispania baada mchezaji huyo raia wa Ubelgiji
kuumia misuli ya paja katika mchezo wa jumamosi wa Ligi Kuu ya
Uingereza dhidi ya Swansea na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne.
Kevin De Bruyn akisikilizia maumivu ya misuli ya paja
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni