.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Septemba 2016

WANAWAKE WATATU WALIOVAMIA KITUO CHA POLISI KENYA WAUWAWA

Wanawake watatu wameuwawa Kenya baada ya kujaribu kufanyashambulizi katika kituo kikuu cha polisi katika mji wa Mombasa.

Wanawake hao waliokuwa wamevalia vazi la hijabu, waliingia katika kituo hicho cha polisi wakisema wanataka kuripoti tukio la kuibiwa simu.

Katika tukio hilo mwanamke mmoja alichomoa kisu, na mwingine alitupa bomo la petroli na kusababisha moto ambapo katika tukio hilo maafisa polisi wawili walijeruhiwa.

Haijafahamika nani haswa amehusika na shambulizi hilo, hata hivyo kundi la wapiganaji wa al-Shabab limekuwa likifanya mashambulizi nchini Kenya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni