.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Septemba 2016

DAKTARI AELEZA KUWA HILLARY CLINTON ANAUGUA NIMONIA

Mgombea urais wa Marekani Bi. Hillary Clinton, amefuta safari yake ya kwenda California, baada ya kubainika kuugua ugonjwa wa nimonia.

Bi. Clinton aliugua jana katika tukio la kumbukumbu ya Septemba 11, na kulazimika kuondoka huku akishikiliwa na walinzi na aliishiwa nguvu na kutaka kuanguka.

Daktari wake Dk. Lisa R Bardack amesema jana usiku kuwa Bi. Clinton alipandwa na joto kali na kuishiwa na maji mwilini akiwa katika kumbukumbu za tukio hilo huko Manhattan. 
                  Bi. Hillary Clinton akisaidiwa na wasaidizi wake kwenda kwenye gari lake
 Bi. Hillary Clinton akikaribia kuanguka baada ya kuishiwa nguvu alipokaribia gari lake

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni