Alex Oxlade-Chamberlain amefunga
mara mbili wakati Arsenal ikipambana kiume na kushinda 2-0 katika mchezo
wa kombe la EFL dhidi ya timu ya Reading.
Kiungo huyo wa Uingereza, alifunga
goli la kwanza kwa kuingia kwenye boksi na kuupiga mpira kwenye kona
ya chini ya goli.
Reading nusura wasawazishe, kwa
shuti Callum Harriott lililogongwa na kupaa juu ya goli.
Oxlade-Chamberlain alifunga goli la pili kwa shuti lililogongwa na
kumpoteza kipa mahesabu.
Alex Oxlade-Chamberlain akifunga goli la kwanza
Alex Oxlade-Chamberlain akiachia shuti lililogongwa na kutinga wavuni na kufunga goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni