Mchezaji nyota mkongwe wa Brazil,
Carlos Alberto, ambaye alikuwa kapteni katika kombe la dunia mwaka
1970 na kuibuka mabingwa, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.
Alberto alifunga moja ya goli bora
katika historia ya kombe la dunia mwaka 1970 dhidi ya Italia kwa
shuti kali la chini.
Beki huyo wa kulia Alberto alikuwa
kapteni wa Brazil mara 53, na pia alishinda ubingwa wa Ligi ya Brazil
akiwa na timu ya Fluminense na Santos, ambapo alicheza michezo 400.
Carlos Alberto akiwa ameshika kombe la dunia hii ilikuwa mwaka 2014
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni