.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

DANIEL STURRIDGE ATUPIA MBILI LIVERPOOL IKITINGA ROBO FAINALI KOMBE LA EFL

Daniel Sturridge amefunga mara mbili wakati Liverpool ikiitoa Tottenham kwa magoli 2-1 na kutinga robo fainali ya kombe la EFL, na kuweka rekodi ya kutofungwa katika michezo 10.

Sturridge ambaye jumamosi aliingia akitokea benchi katika mchezo walioifunga West Brom, jana ilimchukua dakika 10 tu kufunga goli kwa shuti la umbali wa yadi sita.

Divock Origi aliyeonyesha kiwango kizuri alimtengenezea nafasi mbili Sturridge ambaye alizipoteza, lakini baadaye wawili hao walishirikiana vizuri na Sturridge kufunga goli la pili.
                                              Daniel Sturridge akifunga goli la kwanza la Liverpool
                           Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge akifunga goli la pili

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni