Timu ya Arsenal imeongeza pesha kwa
kocha wa Sunderland David Moyes baada ya kupata ushindi mzuri wa
magoli 4-1 dhidi ya timu hiyo na kuifanya iendelee kubakia chini ya
msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika mchezo huo Alexis Sanchez
aliipatia Arsenal goli la kuongoza baada ya kumpita beki Lamine Kone
na kutumbukiza kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Alex
Oxlade-Chamberlain.
Arsenal walioutawala mpira
walijikutwa wakinyimwa penati baada ya Sanchez kuonekana kuangushwa,
na kisha baadaye Jermain Defoe kusawazisha kwa mkwaju wa penati baada
ya kipa Petr Cech kumfanyia madhambi Duncan Watmore.
Hata hivyo Arsenal waliongeza magoli
mengine matatu ya haraka ndani ya dakika sita na sekunde 20,
yaliyofungwa na Olivier Giroud magoli mawili na Sanchezi goli moja.
Olivier Giroud akiwa ameruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliojaa wavuni na kuandika goli
Alexis Sanchez akiwa amempoteza maboya kipa wa Sunderland na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni