Timu ya Manchester City imerejea
kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kishindo baada ya kuiduwaza
West Ham kwa magoli 4-0, na kumaliza kipindi kigumu cha kocha Pep
Guardiola.
Kocha Guardiola alikuwa hajapata
ushindi katika michezo sita kwenye michuano yote, alishuhudia kikosi
chake kikipata goli la kwanza kupitia kwa Sergio Aguero alipofunga
kufuatia mpira wa kurushwa na Ilkay Gundogan.
West Ham walijikuta wakinyong'onyea
zaidi baada ya Aguero kufunga tena akiwaadhibu mabeki waliokuwa
wakisita kumkaba kwa kuachia shuti kali lililojaa kwenye kona ya juu
ya goli.
West Brom walionekana kuimarika
katika kipindi cha pili, lakini walishindwa kuzitumia vyema nafasi
walizozipata, kabla ya Gundogan kuwatungua magoli mawili la kwanza
akipewa pande na Aguero na la pili akilishwa na Kevin de Bruyne.
Mshambuliaji nyota Sergio Aguero akiuangalia mpira alioupiga ukielekea kujaa wavuni
Kocha Pep Guardiola akimkumbatia kwa furaha mshambuliaji wake Sergio Aguero
Wakati Manchester City ikishinda,
majirani zao Manchester United walijikuta wakiwekewa ngumu nyumbani na Burnley
kwa kutoka sare tasa, licha ya kuitawala mno mechi hiyo lakini ngome
ya Burnley ilikuwa imara kulinda goli lao.
Katika mchezo huo kocha Jose Mourinho alijikuta akilazimika kuutazama mchezo huo jukwaani baada ya kukwaruzana refa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni