.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Oktoba 2016

ASKOFU SANGU AMPATIA TANO RAIS MAGUFULI

Askofu Lebaratus Sangu akiongoza harambee akiwa na Mbunge wa Busega, Mh Chegeni ( aliyevaa suti ) 
Askofu Lebaratus Sangu akimpongeza mbunge wa Busega, Dr Chegeni kwa kujitolea kwake. Na Shushu Joel,BUSEGA

ASKOFU wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amemwagia sifa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kwa kusema kuwa ni rais wa mfano wa kuigwa hapa nchini na dunia kwa ujumla.

Hayo ameyasema jana alipokuwa katika harambee ya kufanikisha ujenzi wa kanisa katika kata ya mkula wilaya ya Busega mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa harambee hiyo.

Sangu alisema kuwa JPM ni rais wa pekee sana kwani anajitolea mambo mengi katika kuhakikisha wananchi wa rika la chini nao wanakuwa na sauti ya kusikilizwa na si kama ilivyo kuwa zamani,kwa wanyonge walivyokuwa wakikandamizwa na hivyo sauti zao zilikuwa hazisikiki mahali popote pale.

Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa kwa vitu vingi sana na ambavyo havipatikani nchi zingine, lakini hapa kwetu vinapatikana vitu hivi ni kama amani,upendo na mshikamano tulionao watanzania ambao Mungu alitubariki na kutupatia hekima ya pekee kabisa.

“Hivyo nawaasa watanzania kumuombea rais wetu ili aweze kuendelea kuwatumikia watanzania wote bila kuangalia nafasi aliyonayo hivyo naamini JPM ni rais wa wanyonge” alisema

Pia aliongeza kuwa Tanzania ni tajiri katika raslimali hivyo amewata watanzania kutokutegemea misaada toka nje ya nchi bali sisi kama watanzania tukijituma tutafika mbali na kutimiza malengo yetu ya kila mmoja kuwa na hali ya saizi ya kati.

"Kutegemea misaada na sawa na kuwa na uhuru pasipo kuwa huru hivyo tukijituma kwa kufanya kazi kwa bidii ni lazima tutafika mbali na kila mmoja akitimiza wajibu wake kwa kujitambua na kuthamini kazi anayoifanya basi nchi yetu itafika mbali kwa kuwa na kipato kikubwa, alisema.

Katika harambee hiyo iliyoudhrliwa na mbunge wa jimbo la Busega Dr Rafael Chegeni ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi ilifanikiwa kupata million 19.6 pesa taslimi kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Mbali na upatikana wa pesa hizo Askofu huyo pia amempongeza Chegen kwa utendaji mzuri wa kazi kwa wananchi wake wa Busega na kumshauri zaidi aweze kuhakikisha kundi la vijana analiangalia kwa jicho la tatu katika kulifanikishia upatikanaji wa vitendea kazi zao za ujasiliamali.

Chegen mpaka sasa amepeleka vijana 15 nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kujifunza vitu mbalimbali wakiwemo 5 waliokwenda nchini china kwa ajili ya kujifunza lugha hiyo ili waweze kuwa wakalimani pindi wageni hao watapokuwa hapa nchini kwa malengo ya kutafuta uwekezaji,huku kundi jingine wakijifunza shughuli mbalimbali za kijamii ambao watakuja jimboni kuwapatia somo wenzao ambao hawajaenda huko, huku lengo likiwa ni kuondoa kero ya upatikanaji wa ajira katika jimbo langu alisema Chegen

Askofu pia amewapongeza wananchi wote kwa kulinda alama ya taifi hili ambayo ni amani na kuwataka kuendeleza kuilinda kwani machafuko tunayoyaona nchi za mbali ni aibu kwa mungu na laana pia.



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni