Bilionea wa Makasino, James Packer,
ametengana na mchumba wake mwanamuziki nyota wa zamani nchini
Marekani Mariah Carey.
Kwa mujibu wa jarida la Australian
la Woman's Day, Packer, 48, amemtosa nyota huyo wa pop, 46, kutokana
na kuwa na matumizi makubwa pamoja na kuwa na shoo yake ya maisha ya
uhalisi ya Mariah inayoonekana duniani.
Kwa mujibu wa jarida hilo hata hivyo
Packer, amemruhusu Mariah kuendelea kubakia na pete ya uchumba ya
almasi yenye thamani ya dola milioni 10, sawa na karibu shilingi
bilioni 22 za Tanzania.
Mariah Carey akiwa amevaa pete ya uchumba ya madini ya almasi yenye thamani ya dola milioni 10
Bilionea James Packer akiwa na mchumba wake Mariah Carey kabla ya penzi halijatumbukia nyongo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni