Bingwa wa dunia wa kurusha mkuki,
Julius Yego, yupo katika hali nzuri na anafanyiwa vipimo katika
hospitali ya Eldoret, Kenya baada ya kupata ajali akiwa na gari lake
jana usiku.
Yego alipata ajali hiyo akiwa
anaendesha gari aina ya Toyota Prado kwenye barabara Kapsoya karibu
na Benki ya Equity majira ya saa nne usiku.
Gari hilo limeharibika vibaya sehemu
ya mbele, limeegeshwa kituo cha polisi kati cha Eldoret, huku polisi
waliokuwa zamu usiku wakizuia watu kulipiga picha gari hilo.
Julius Yego akijiandaa kurusha mkuki


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni