Mtoto wa kike wa bingwa wa zamani wa
riadha, Tyson Gay, ameuwawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la
Kentucky nchini Marekani.
Polisi wa Lexington wamesema binti
huyo Trinity Gay, 15, alipigwa risasi shingoni wakati wa tukio la
kutupiana risasi kutoka kwenye magari mawili kwenye maegesho ya hoteli.
Binti huyo alikimbizwa hospitali,
lakini baadaye ilielezwa kuwa amefariki dunia. Gay ambaye anatokea
mji wa Lexington amethibitisha kifo cha binti yake huyo.
Tyson Gay akiwa na binti yake Trinity aliyeuwawa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni