Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, Kulia, akiwahutubia wahitimu na jumuiya ya Bodi ya
taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) (Hawako Pichani),
wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika katika Kituo cha
Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi
Mtendaji wa NBAA, Bw. Pius Maneno na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na
Mafunzo wa Bodi hiyo, Bi. Anne Mbughuni.
Baadhi ya wahitimu wa taaluma ya juu
ya uhasibu (CPA), wakiwa tayari kutunukiwa shahada zao na Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, katika Mahafali ya 38
yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi
wa Hesabu (NBAA) kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam. (Picha zote na Wizara ya Fedha)
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango, akimkabidhi cheti cha kufanya vizuri katika masomo ya
taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T), Bi. Happiness Ngowi, wakati wa
mahafali ya 38 ya Bodi hiyo yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya
Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), kilichopo Bunju, nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango, akitangaza kuwatunuku vyeti wahitimu wa taaluma ya juu
ya uhasibu (CPA-T) waliofanya vizuri katika masomo yao, wakati wa
mahafali ya 38 ya NBAA, yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa
ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, kilichopo Bunju, nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam.
Wahitimu waliofanya vizuri katika
masomo ya NBAA, baada ya kupokea vyeti vya kutambua umahili wao
katika masomo pamoja na kupewa zawadi za fedha taslimu zilizotolewa
na wadhamini mbalimbali wa Bodi hiyo, wakati wa Mahafali ya 38
yaliyofanyika katika Kituo cha NBAA, kilichoko Bunju, nje kidogo ya
Jiji la Dar es salaam.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya Juu
ya Taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu CPA-T, inayotolewa na Bodi
ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), wakila
kiapo cha utii na uadilifu wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo,
yaliyofanyika katika kituo kilichoko Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar
es salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango, (aliyeketi nafasi ya saba kutoka kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi wa Bodi pamoja na wadhamini wa tuzo
mbalimbali zilizotolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo
yao, tukio lililofanyika katika kituo cha NBAA, kilichoko Bunju, nje
kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Prof. Isaya
Jairo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Pius Maneno,
wakiondoka kwenye viwanja vya mahafali baada ya kumaliza kuwatunuku
vyeti na shahada mbalimbali wahitimu wa kozi mbalimbali za NBAA,
katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango (kushoto), akisalimiana na Msajili wa Hazina Bw.
Laurance Mafuru, baada ya kumalizika kwa mahafali ya 38 ya Bodi ya
taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA), yaliyofanyika katika
kituo cha Bodi hiyo, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni