Bondia David Haye anajipanga
kupambana katika pambano la uzito wa juu mwakani, huku akitarajiwa
kuwania mkanda wa uzito huo wa WBO.
Joseph Parker na Andy Ruiz
watapambana huko Auckland Desemba 10 mwaka huu, kuwania mkanda huo
ulioachiwa na Tyson Fury, na Haye atakuja kupigana na mshindi wa
pambano hilo.
Haye alitwaa ubingwa wa uzito wa juu
wa WBA baada ya kumpiga bondia mwenye mwili mkubwa Mrusi Nikolai
Valuev mwaka 2009 kabla ya kuupoteza kwa Wladimir Klitschko.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni