Bondia Tony Bellew, ametetea taji
lake la dunia WBC kwa kumdunda kwa KO BJ Flores katika raundi ya
tatu, na kumtaka David Haye kupambana naye.
Bondia huyo Muingereza Bellew
alimdondosha Mmarekani BJ Flores mara tatu kwa kutumia ngumi yake
kali ya mkono wa kushoto katika raundi ya pili, Jijini Liverpool.
Baada ya kumdunda JB Flores, Bellew
alianza kupaza sauti za kumtaka Haye apande ulingoni huku akimponda
jambo ambalo karibu lisababishe mabondia hao kuzipiga.
Tony Bellew akimtwanga ngumi nzito ya mkono wa kushoto JB Flores
JB Flores bondia ambaye ni rafiki wa David Haye akianguka chini baada ya ngumi kumuingia vilivyo
Bondia Tony Bellew akimpiga mkwara bondia David Haye mwenye afro
Bondia Tony Bellew akishuka ulingoni kumfuata David Haye ili wazichape
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni