Mwanana wa mfalme wa Thailand, Maha
Vajiralongkorn, anataka maziko ya mfalme wa nchi hiyo kwa mwili wake
kuchomwa moto kuhairishwa japo kwa mwaka mmoja.
Mfalme Bhumibol Adulyadej alifariki
dunia siku ya Alhamisi, lakini mwanaye anayetarajiwa kumrithi anataka
kupatiwa muda zaidi wa maombolezo ya baba yake.
Kwa sasa Waziri Mkuu Prayuth
Chan-ocha anatarajiwa kuwahakikishia wananchi wa Thailand kuhusiana
na mrithi wa mfalme Bhumibol.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni