Wananchi wa Haiti wenye hasira
wamepora misaada kwenye magari, wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa akitembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga
Matthew, kilichouwa watu 900 nchini humo.
Bw. Ban Ki-moon amesema ameshuhudia
tukio la kuporwa misaada akiwa Les Cayes, ambapo ameahidi misaada
zaidi kwa Haiti, na kuyaomba mataifa mbalimbali duniani kutoa misaada
zaidi.
Takwimu zinaonyesha zaidi ya watu
milioni 1.4 nchini Haiti wanahitaji misaada ya kibinadamu ya haraka,
huku kukiwa na hofu ya kutokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Wananchi wenye hasira wakikwaruzana na watoa misaada
Hasira za wananchi wenye kuhitaji misaada zimeibua mapambano katika kambi za misaada za Umoja wa Mataifa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni