Nyota wa Real Madrid, Raphael
Varane, Karim Benzema, Marcelo, Isco and Cristiano Ronaldo
wamezifumania nyavu wakati ikiibuka na ushindi mnono wa magoli 6-1
dhidi ya Real Betis.
Katika mchezo huo wa La Liga
ulioirejesha Real Madrid katika nafasi ya juu, Raphael Varane alikuwa
wa kwanza kufunga goli kwa mpira wa kichwa alioupiga kifundi.
Karim Benzema aliongeza goli la pili
kwa kikosi hicho cha Zinedine Zidane, na kisha Marcelo kuongeza la
tatu huku Isco akifunga la nne na la tano kisha Ronaldo akikamilisha
la sita.
Karim Benzema akishangilia kwa kukimbia baada ya kufunga goli
Cristiano Ronaldo akidokoa mpira na kufunga goli la sita kwa Real Madrid
Katika mchezo mwingine Yannick
Carrasco amefunga magoli matatu yaani hat-trick, wakati Atletico
Madrid ikitokea nyuma kwa kufungwa goli moja na kuibuka na ushindi wa
magoli 7-1 dhidi ya timu iliyomkiani ya Granada na kuongoza ligi ya
La Liga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni