Tyson Fury ameachia mikanda yake ya
ubingwa wa uzito wa juu ya WBO na WBA, kutokana kuwepo katika kipindi
cha matibabu ya msongo wa mawazo.
Muingereza huyo, 28, alikiri kutumia
dawa za kulevya aina ya cocaine ili kukabiliana na msongo wa mawazo
na inaelekea huenda akapoteza leseni yake ya ngumi.
Fury hakupigana tangu ampige
Wladimir Klitschko Novemba mwaka 2015 na alijiondoa mara mbili
kushiriki mapambano ya kurudiana na Klitschko.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni