Timu ya taifa ya Brazil imeweza
kuongoza katika kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia 2018 kwa
mataifa ya Amerika ya Kusini, baada ya kushinda magoli 2-0 dhidi ya
Venezuela katika mchezo uliochezwa huku mvua zikinyesha na kusimama
kwa nusu saa katika dimba la Merida.
Mabingwa hao mara tano wa kombe la
dunia ambao walicheza bila mshambuliaji wao Neymar walipata goli la
kwanza ndani ya dakika nane ambalo lilionekana lilitokana na mzaha na
kufungwa vizuri.
Kipa wa Venezuela Daniel Hernandez
alijaribu kumpasia mpira beki wake lakini, Gabriel Jesus aliuwahi na
kisha kuunyanyua mpira juu ya kipa huyo kwa umbali wa mita 20 na
kufunga goli zuri. Willian alifunga goli la pili la Brazil.
Mchezaji wa Chelsea Willian akiifungia Brazil goli la pili
Mashabiki wakitumia tochi za simu zao kupata mwanga baada ya taa kuzimika kwenye uwanja wa Merida
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni