Uingereza inapaswa kushukuru umahiri
wa kulinda goli wa kipa Joe Hart na kuwa na bahati kwa kiasi fulani
baada ya kuambulia sare tasa dhidi ya Slovenia, katika mchezo wa
kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia 2018.
Hart ambaye anachezea kwa mkopo
Torino, ambaye alionekana kama asiyehitaji Manchester City, amemuokoa
na aibu kocha wa muda Gareth Southgate ya kupoteza mchezo wa jana kwa
timu ambayo ni ya 67 katika viwango vya soka duniani.
Hart alimnyima magoli Josip Ilicic
baada ya kupigiwa pasi mbovu na Eric Dier na Jordan Henderson, lakini
kali zaidi aliyotoa kipa huyo ni pale alipopangua mpira wa kichwa wa
Jasmin Kurtic na kuutoa nje katika kipindi cha pili.
Kipa Joe Hart akiruka juu na kupangua mpira kwa mkono wa kushoto
Kipa Joe Hart akianguka chini baada ya kupangua mpira na kuutoa nje
Homa ya mchezo ilipanda kiasi cha kujikuta wachezaji wakitaka kuzichapa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni