Kocha Jose Mourinho amepata
makaribisho ya aibu wakati akirejea Chelsea baada ya klabu yake hiyo
ya zamani kuichakaza Manchester United magoli 4-0 katika dimba la
Stamford Bridge.
Chelsea ambao walimtimua Mourinho
mwaka jana, waliongoza kwa kupata goli ndani ya sekunde 30, baada ya
Pedro kutumia udhaifu wa beki na kutumbukiza mpira kimiani.
Gary Cahill aiongeza la pili baada
mpira wa kona ya Eden kugonga mwamba na kurudi katika eneo la goli,
na kisha baadaye Hazard akafunga la tatu na N'Golo Kante kufunga la
nne.
Pedro akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza
Gary Cahill akipiga mpira uliomshinda kipa David de Gea na kuandika goli la pili
Kocha Jose Mourinho akimnong'oneza kitu kocha wa Chelsea Conte mara baada ya kumalizika mpira




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni