Timu ya Chelsea imeendelea kukwea
vyema kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza na kushika nafasi ya
nne, baada ya kuifunga Southampton magoli 2-0.
Chelsea ilijipatia goli lake la
kwanza kupitia kwa Eden Hazard, akitumia fursa ya kukaba kiuzembe na
kumpita Steven Davis, kisha kuachia shuti lililompita tobo kipa
Fraser Forster.
Southampton walipata nafasi za
kutosha lakini walishindwa kulitikisa goli la Chelsea ambao walioneka
kuwa tishio. Diego Costa alifunga goli safi kwa shuti la kuzungusha
la yadi 22.
Diego Costa akiachia shuti la kuzungusha lililozaa goli la pili la Chelsea
Eden Hazard akionyesha hisia zake baada ya kukosa goli katika moja ya shambulizi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni