Timu ya Everton imemaliza ukame wa
kutoshinda mechi tano mfululizo baada ya kupata ushindi dhidi ya West
Ham ambayo inaendelea kujikita chini ya msimamo wa ligi.
Katika mchezo huo Romelu Lukaku
aliipatia Everton goli la kwanza kwa mpira wa kichwa wa karibu na
goli na kufikisha magoli saba katika ligi kuu aliyowahi kuifunga West
Ham.
Everton iliendelea kuimarika kadri
muda ulivyoenda na kujipatia goli kupitia kwa Ross Barkley,
akiunganisha mpira uliopigwa na Lukaku.
Romelu Lukaku akifunga goli la kwanza la Everton kwa kichwa
Ross Barkley akiunganisha pande alilopewa na Lukaku na kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni