Chelsea imewachakaza magoli 3-0
mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City na kuifanya
kukubali kipigo cha nne mfululizo wakiwa ugenini.
Katika mchezo huo uliopigwa Stanford
Bridge Chelesa waliutawala na katika dakika ya saba Nemanja Matic
aliugonga mpira wa kona ya Eden Hazrad na Diego Costa kufunga goli.
Mpira wa adhabu uliopigwa na David
Luiz uligonga mwamba na kumkuta Pedro aliyemgongea Hazrad ambaye
aliuzungusha na kumshinda kipa Kasper Schmeichel.
Luiz pia aligonga mwamba wa goli
lake kwa mpira wakati akijaribu kuokoa, hata hivyo baadaye Victor
Moses alifunga la tatu baada ya kugongeana vyema na Nathaniel
Chalobah.
Mshambuliaji Diego Costa akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza
Eden Hazard akishangilia goli kwa kuonyesha ishara ya kuungana na Willian aliyempoteza mama yake kwa ugonjwa wa saratani
Victor Moses akiruga sarakasi kushangilia goli lake alilofungwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni